Waziri Mkuu Majaliwa azindua shule ya Sekondari maalum ya wavulana Nachingwea

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Kaimu Mhandisi wa wilaya ya Nachingwea, Misoji Sahani ambaye  alitoa maelezo kuhusu michoro ya Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana  Nachingwea  kabla ya  Waziri Mkuu kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Oktoba 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Kaimu Mhandisi wa wilaya ya Nachingwea, Misoji Sahani (Kulia) baada ya kuvutiwa ubora na viwango vya hali ya juu vya ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana Nachingwea ambayo ujenzi wake umesimamiwa na Mhandisi huyo. Mheshimiwa Majaliwa pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Oktoba 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalum  ya Wavulana Nachingwea, Oktoba 25, 2021. Kulia ni Mbunge wa Nachingwea , Dkt. Amandus Chingwile na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Muonekano wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wavula Nachingwea ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake, Oktoba 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhandisi wa wilaya ya Nachingwea, Misoji  Sahani   (kulia) kuhusu  ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana Nachingwea kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Oktoba 25, 2021.  Wa tatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Lindi,  Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




 

Post a Comment

0 Comments