Ticker

6/recent/ticker-posts

Bodi ya Tumbaku yawapongeza wazawa

 


Bodi ya Tumbaku nchini inathamini mchango wa kampuni ya wazawa ya ununuzi wa tumbaku ikisema yanajitahidi kutoa mchango wao katika sekta ya Tumbaku.


 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Nchini, (TTB), Stan Mnozya,amesema kampuni Za wazawa pamoja na changamoto walizonazo,bado mchango wao ni mkubwa katika sekta ya Tumbaku.


"Kampuni za ununuzi wa tumbaku ya wazawa,zimekuwa zikikabiliwa na changamoto kadhaa lakini hasa mitaji na sisi kama bodi tunataka ziimarike zaidi"Amesema


Mnozya ameeleza kuwa kwa msimu huu,makampuni ya wazawa,yamenunua kilo milioni 9 za tumbaku zenye thamani ya Sh27bilioni na kuwa tayari yamelipa zaidi ya Sh22bilioni.


Mchango wao ni zaidi ya asilimia kumi katika manunuzi kwani jumla ya Tumbaku ni kilo 68 milioni  zimenunuliwa zenye thamani ya zaidi ya Sh200bilioni.


Amesema mchango wa kampuni za wazawa hauwezi kubezwa kwani zilianza biashara ya ununuzi wa tumbaku msimu uliopita na msimu huu ni mwaka wao wa pili na kuwa Wana uhakika msimu ujao watafanya vizuri zaidi na kuwalipa wakulima kwa wakati.


Mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni mojawapo ya wazawa ya ununuzi wa tumbaku PCL,Ahazi Itika,amesema kama wakiungwa mkono na vyombo vya fedha na Serikali kwa kupatiwa mikopo,watafanya Mambo makubwa.


"Tumeweza kulipa kiasi kikubwa Cha fedha Tena bila kuwa na.mikopo,he tukiwa na mikopo so itakuwa vizuri zaidi?"Ameeleza.


Ahazi amekiri makampuni ya wazawa kukabiliwa na changamoto hasa mitaji lakini pamoja na hayo kuwa wanajitahidi na wanapaswa kuungwa mkono na Kila mpenda maendeleo ya Nchi na sekta nzima ya Tumbaku.


Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha wakulima wa tumbaku Manyoni,Amos Ngayaula,amewapongeza makampuni ya ununuzi wa tumbaku ya wazawa,Akisema yanafanya kazi nzuri pamoja na ugeni wao katika Biashara ya Tumbaku.


Ameeleza kuwa wao kwa miaka mitatu walishindwa kulima tumbaku kutokana na kutopewa makisio na makampuni ya kigeni lakini kwa jitihada za bodi ya Tumbaku na makampuni ya wazawa,wameanza uzalishaji msimu huu na msimu ujao watakuwa vizuri zaidi.

Post a Comment

0 Comments