IAEA yasema hakuna maendeleo katika mazungumzo ya nyuklia na Iran

 


Vienna, Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya Atomiki IAEA limesema hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika katika mazungumzo na Iran juu ya kufuatilia shughuli zake za nyuklia, siku chache kabla ya kuanza tena kwa mazungumzo ya kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015. 


Mkuu wa shirika hilo la nishati ya Atomiki Rafael Grossi ameuambia mkutano wa bodi hiyo kwamba, mazungumzo aliyoyafanya mjini Tehran licha ya kuwa mazuri lakini hawakufikia makubaliano. 


Grossi alikuwa Tehran kwa ajili ya kutafutia ufumbuzi masuala kadhaa ikiwemo kutaka shirika la IAEA kupewa nafasi ya kuyafikia maeneo ya vinu vya nyuklia ya Iran, na kulalamikia jinsi waangalizi wake wamekuwa wakilazimika kupitia ukaguzi usioridisha. 


Behrouz Kamalvandi, msemaji wa shirika la nishati ya Atomiki la Iran ameliambia shirika la habari la serikali kuwa, wamefanya mazungumzo hadi dakika ya mwisho lakini bado kuna kazi zaidi ya kufanywa.

Post a Comment

0 Comments