Putin asema silaha za kijeshi nchini Ukraine ni mstari mwekundu


Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema hivi leo kwamba utanuzi wa miundombonu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO nchini Ukraine ni mstari mwekundu ambao alitarajia usingevukwa. 


Akizungumza kwenye jukwaa la uwekezaji mjini Moscow, Putin alielezea wasiwasi wake juu ya mafunzo ya kijeshi yanaofanyika karibu na mipaka ya nchi yake. Putin alisema pia kwamba nchi yake inatengeneza kombora jipya linalosafiri kwa kasi ambalo karibuni litakuwa kwenye ghala lake la silaha. 


Kauli ya Putin inakuja muda mfupi baada ya Marekani na Uingereza kuonya dhidi ya kile zilichosema ni uchokozi mpya wa kijeshi wa Urusi dhidi ya Ukraine, wakati NATO ikikutana kuzungumzia dhamira ya Urusi kuweka kiwango kikubwa cha wanajeshi kwenye mpaka wake na Ukraine.

Post a Comment

0 Comments