Shambulio la kujitolea muhanga dhidi ya msafara wa usalama Somalia lawauwa wanane

 


Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, televisheni ya taifa imeripoti.


Watu wapatao 17 wamejeruhiwa, wakiwemo watoto 13 kutoka shule jirani nae neo la tukio.


Mlipuaji mabomu wa kujitoa mhanga wa kikundi cha al-Shabab aliyekuwa anaendesha gari lililosheheni vilipuzi alilenga msafara wa kampuni ya usalama ya kibinafsi, Duguf, ambayo ilipewa kandarasi ya kulinda Umoja wa mataifa.


Polisi haikusema iwapo wafanyakazi wa Umoja wa mataifa waliumia katika shambulio hilo.


Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa mlipuko huo ulitokea wakati wa msongamano wa magari karibu na makutano yanayofahamika kama -Kilometre Four junction.


Kundi lenye uhusiano na al-Qaeda la wanamgambo wa al-Shabab limethibitisha kutekeleza shambulio hilo. Vyanzo vya habari vinavyounga mkono al-Shabab media vimesema wanamgambo hao waliwalenga “maafisa wa kijeshi wazungu”.


Mara kwa mara Al-Shabab wamekuwa wakiwalenga maafisa wa vikosi vya usalama na serikali mjini Mogadishu.



Post a Comment

0 Comments