Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Tabia zitakazokusaidia kuwa mshindi katika maisha yako

 

Najua umekuwa ukijifunza mara kwa mara na unatambua umuhimu wa tabia katika kufikia mafanikio makubwa. Kama ambavyo tumekuwa tukijifunza kwenye baadhi ya makala kuwa tabia zina nguvu kubwa sana ya kuweza kubadilisha maisha yako isipokuwa inategemea umebeba tabia za aina gani.

Mara nyingi tumekuwa tukiona watu wenye mafanikio wamefikia hapo kutokana na tabia zao za kimafanikio. Na watu maskini pia wamekuwa hivyo kutokana na kung’ang’ania kila siku tabia za kimaskini zinazowarudisha nyuma. Hivyo ni lazima wewe kujijengea tabia za mafanikio ili kuweza kufanikiwa.

Tabia za watu wenye mafanikio  zitakazokusaidia kuwa mshindi katika maisha yako.

1. Wanatimiza ahadi walizojiwekea, ikiwa pamoja na mipango na malengo yao.

2. Ni watu wa kujichanganya na watu chanya.

3. Ni watu wa kufanya kila linalowezekana mpaka wanatimiza malengo yao waliyojiwekea.

4. Wanajua namna ya kutengeneza timu bora ya mafanikio.

5. Siku zote wanatafuta njia bora ya kuwafikisha kwenye mafanikio makubwa.

6. Ni watu wa kujifunza kila siku kwa kujisomea au kuhudhuria semina mbalimbali.

7. Ni watu wa kutoahirisha mapema mipango waliyojiwekea.

8. Ni watu wa kutafuta fursa hata pale wengine wanapoona kuna vikwazo.

9. Ni watu wa kujifunza sana, hasa pale wanapokosea.

10. Wanafanya mambo yao kwa umakini .

11. Ni watu wasiotawaliwa na hofu zisizo na maana kwao.

12. Ni watu wa kuwajibika na hawapotezi muda wao kulalamikia watu wengine.

13. Hawa sio watu wa kuacha jambo na kuanza jambo lingine tena kila wakati.

14. Hukabilana na changamoto zinazojitokeza bila woga.

15. Wanafanya mambo ambayo kwa wengine siyo rahisi kwa wengine kuweza kufanywa.

16. Ni watu wa kwasaidia wengine, kuweza kufikia malengo yao makubwa waliyojiwekea.

17. Siku zote wanawekeza kwenye maeneo wanayoyamudu na sio kinyume cha hapo.

18. Mara nyingi ni watu ambao hawahitaji kusifiwa ili waweze kuendelea kufanya kile wanachokifanya.

19. Ni watu wa kujirekebisha kila siku kupitia maisha ya kila siku.

20. Ni watu wanaoongozwa na kuendelea kuzifatilia ndoto zao kila siku bila kuchoka.

Je, unatabia za kimafanikio ambazo zinazoweza kukuongoza kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako yote? Kwa ufupi, hizo ndizo tabia ambazo wanazo watu wenye mafanikio na kuzitumia kufanikiwa siku hadi siku.

Post a Comment

0 Comments