Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 25.11.2021


Mshambuliaji wa Paris St-Germain na France Kylian Mbappe, 22, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo wakati kandarasi yake itakapokwisha msimu wa ujao , huku Newcastle united ikiwa miongoni mwa klabu ambayo inawaza kumuwania mchezaji huyo mshindi wa kombe la dunia.(Express)

Winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 28, na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 25, wanaonekana kama wachezaji mbadala wa winga wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26, wanaotarajiwa kujiunga na Barcelona mwezi Januari.(ESPN)

Wito wa Manchester United kutaka kumuajiri mkufunzi wa klabu ya PSG Mauricio Pochettino umekataliwa na klabu hiyo . (Manchester Evening News)


Meneja huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Pochettino , 49 atalazimika kusubiri miezi sita kabla ya kuweza kuwa mkufunzi wa Man United.. (Star)

Mkufunzi wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Lucien Favre na mkufunzi wa Lyon Rudi Garcia wamehojiwa na United kuhusu kuwa mufunzi wa muda katika klabu hiyo.. (Telegraph)

Ralf Rangnick, aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa klabu ya RB Leipzig na aliyekuwa mkufunzi wa Roma Paulo Fonseca wote wako katika orodha hiyo.. (Mail)

Picha ya aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United Olegunnar Solskjaer imeondolewa katika uwanja wa Old Trafford. (Sun)



Liverpool na Barcelona zinamuwania mshambuliaji wa Chelsea Christian Pulisic, 23, lakini The Blues haiwezi kumuuza mchezaji huyo kwa timu yoyote ya Ligi ya Premia huku klabu hiyo ya Uhispania ikiwa haina uwezo wa kutoa dau la Yuro 50m linalohitajika ili kumsaini winga huyo wa Marekani.. (El Nacional, in Catalan)

Chelsea imefanya mazungumzo na beki wa klabu ya Fenerbahce na Hungary Attila Szalai, 23. (Football Insider)

Wolves itasikiliza maombi ya kumuuza wing wa Uhispania Adama Traore, 25, mwezi Januari. (Football Insider)


Mashabiki wa Real Madrid wamemkera mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, kulingana na ajenti wake Jonathan Barnett. Bale, 32, ana kandarasi na Real Madrid hadi majira yajayo ya joto. (Marca)

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, ananyatiwa na Atletico Madrid, Barcelona, Newcastle na AC Milan. Kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu . (Calciomercato)

Post a Comment

0 Comments