Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 22.11.2021


Mkufunzi wa Paris St-Germain na raia wa Argentine Mauricio Pochettino ndio mkufunzi nambari moja anayenyatiwa sana na klabu ya Man United ili kuchukua kazi hiyo msimu ujao. Mkufunzi mkuu wa Ajax na raia wa Uholanzi Erik ten Hag yupo katika nafasi ya pili miongoni mwa wakufuni wanaotafutwa na klabu hiyo. (Sky Sports)


Na aliyekuwa mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema kwamba yuko huru kujiunga na mashetani hao wekundi msimu ujao wa joto.. (Telegraph)


Ten Hag alijibu uvumi kwamba atachukua mahala pake Ole Gunnar Solskjaer katika klabu ya Man United kwa kusema kwamba hajasikia ombi lolote kutoka kwa klabu hiyo. (Manchester Evening News)


Wakala wa Kireno Jorge Mendes anaisukuma Man United kujaza pengo la Ole Gunnar Solksjaer kwa kumuajiri mkufunzi wa Sevilla Julen Lopetegui. Raia huyo wa Uhispania ana kandarasi na klabu hiyo hadi 2024 lakini Mendes ambaye anamuwakilisha Cristiano Ronaldo anamtaka kuchukua kazi hiyo Old Trafford. (Manchester Evening News)


Mkufunzi wa Uhispania Luis Enrique amekana madai yanayomuhusisha na klabu ya Manchester United. (Goal)


Real Madrid ina hamu ya kumsajili kiungo wa Chelsea na England Mason Mount. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo katika mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya , ijapokuwa inasemekana anahisi hapendwi na huenda akajiandaa kuondoka. Klabu za Manchester City na Bayern pia zina hamu naye.. (Fichajes - in Spanish)Mkufunzi mpya wa klabu ya Aston Villa Steven Gerrard anataka kumsaini beki wa kushoto wa Croatia Borna Barisic, 29, kutoka klabu yake ya zamani Rangers. (Daily Record)


Mkufunzi wa Everton Rafael Benitez anasema kwamba klabu hiyo itahitaji kuwasaini wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku winga wa England Demarai Gray, 25, akiwa mchezaji wa hivi karibuni kupata jeraha wakati wa mechi waliopoteza kwa Mchester City.. (Liverpool Echo)Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi, 34, hana mpango wa kurudi Barcelona baada ya rais wa klabu hiyo Joan laporta kusema kwamba klabu hiyo ya Uhispania inaweza kumsajili raia huyo wa Argentina katika siku za usoni.. (AS)


Mkufunzi mpya wa Barcelona Xavi ana hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Algeria Baghdad Bounedjah ,29 kutoka klabu ya zamani ya Al-Sadd nchini Qatar. (Sport - in Spanish)Post a Comment

0 Comments