Ticker

6/recent/ticker-posts

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa mafupi

 


Maafisa wa Korea Kusini na Japan wamesema kuwa Korea Kaskazini imefanya jaribio la kombora la masafa mafupi. Hii ni mara ya tatu nchi hiyo yenye silaha za nyuklia kufanya majaribio ya silaha katika kipindi cha wiki moja. 


Mkuu wa majeshi wa Korea Kusini, amesema Korea Kaskazini imefyatua kombora hilo kuelekea upande wa mashariki, bila kutoa maelezo zaidi. Mlinzi wa pwani wa Japan amesema wamegundua kurushwa kwa kombora kutoka Korea Kaskazini katika kile kinachoonekana kuwa kombora au makombora na wanaendelea kuchunguza kubaini kama ni moja au mengi. 


Licha ya kuwekewa vikwazo vya kimataifa kutokana na mpango wake wa silaha za nyuklia, Korea Kaskazini tayari imeshafanya majaribio mawili ya makombora ya masafa marefu tarehe 5 na 11 Januari, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments