Merkel akataa wadhfa aliopendekezewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa


 Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel ameikataa kazi aliyokuwa amependekezewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. 

Afisi ya Merkel imeliambia shirika la habari la dpa leo kwamba, Merkel alizungumza na Katibu huyo Mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki iliyopita, akamshukuru na kumfahamisha kwamba hatoichukua nafasi aliyokuwa amempendekezea. 

Kulingana na duru za Umoja wa Mataifa, Guterres, alikuwa amemuomba Merkel achukue uenyekiti wa bodi ya ushauri inayoongozwa na marais wa zamani. 

Merkel mwenye umri wa miaka 67 hakugombea tena nafasi ya ukansela katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani Septemba iliyopita baada ya kuongoza kwa miaka 16. 

Hakufichua mengi kwa umma kuhusiana na atakayofanya baada ya kustaafu.


Post a Comment

0 Comments