Ticker

6/recent/ticker-posts

Urusi inatarajia mazungumzo na Marekani yataanza tena


Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema ana matumaini kwamba mazungumzo ya usalama kati yake na Marekani yataanza tena baada ya mikutano kadhaa iliyofanyika wiki hii. Lavrov amesema leo kuwa hata hivyo, suala hilo litategemea jibu la Marekani kuhusu mapendekezo ya Urusi.


Urusi ambayo imezitia wasiwasi nchi za Magharibi baada ya kupeleka wanajeshi wake karibu na Ukraine, imetoa masharti kadhaa kuhusu usalama wake ambayo imetaka kuhakikishiwa kisheria na Marekani na Jumuia ya Kujihami ya NATO. 


Urusi imesema kuwa inatarajia kupata majibu ya maandishi kuhusu mapendekezo yake wiki ijayo. Lavrov amesema Urusi inaweza kupeleka vifaa vya kijeshi karibu na Ukraine iwapo mazungumzo ya usalama na mataifa ya Magharibi yatakwama. 


Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock ataizuru Ukraine na Urusi wiki ijayo kuzungumzia mvutano unaoongezeka katika mpaka wao.

Post a Comment

0 Comments