https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wabunge 11 wawasilisha barua za kutokuwa na imani na Boris Johnson | Muungwana BLOG

Wabunge 11 wawasilisha barua za kutokuwa na imani na Boris Johnson

 


Gazeti la The Telegraph linaripoti kuwa wabunge 11 wa chama cha Kihafidhina cha Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson wamewasilisha barua za kutokuwa na imani na kiongozi huyo hii leo. 

Kisheria ni barua 54 za wabunge wa chama hicho zinazohitajika ili kutekeleza kura hiyo isiyokuwa na imani kwa Johnson. 

Kiongozi huyo aliichukua nafasi hiyo ya waziri mkuu mwaka 2019 ili kuukamilisha mchakato wa Brexit kwa kushinda viti vingi katika kipindi cha miaka 30 ila sasa anakabiliwa na shinikizo la kuachia ngazi baada ya ufichuzi kuhusiana na sherehe za kunywa pombe zilizoandaliwa katika makazi na afisi yake ya namba 10 Downing Street kipindi nchi ilipokuwa imefungwa kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. 

Johnson ameomba radhi mara kadhaa kuhusiana na sherehe hizo akisema alikuwa hafamu zilipokuwa zikifanyika.


Post a Comment

0 Comments