Ticker

6/recent/ticker-posts

Watendaji Wa Serikali Za Mitaa (Sheha0 Watakiwa Kufanyakazi Na Kuondoa Muhali

 
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR

WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,  Masoud Ali Mohammed amewataka Watendaji wa Serikali za Mitaa wakiwemo masheha kuondoa muhali katika utekelezaji wa majukumu Yao ili kuleta ufanisi mzuri  katika shehia na mitaa yao.


Wito huo ameutoa leo wakati wa Uzinduzi wa Vitambulisho Maalum vya Masheha wa Wilaya Tatu za Unguja Kaskazin A na B pamoja na Magharib A katika Ukumbi wa Skuli ya Bumbwini.


Waziri Masoud amesema kuwa, ni wajibu Kwa  masheha kufanya kazi kwa uzalendo na kwa mujibu wa sheria ili kuwa waadilifu katika  kuondoa vitendo vya uvunjifu wa amani katika shehia zao.


Hata hivyo Waziri Masoud amesema, vitambulisho hivyo ni nyenzo ambayo itasaidia kufanya  kazi kwa kujiamini katika kazi zao za kuwatumikia wananchi.


Nae  Mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud amesema vitambulisho hivyo ni kielelezo cha kutambulika na kuheshimika na kwamba vitumike vizuri na isiwe chanzo cha kuleta migogoro na wananchi. 


Kwa Upande wao Masheha, wameeleza kuwa wamepata nguvu mpya kwa kupatiwa vitambulisho na watafanyakazi kwa kujiamini katika shehia zao.

Post a Comment

0 Comments