Waziri Mkuu wa Uingereza Johnson asema hatojiuzulu

 


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anayepigania kuinusuru kazi yake baada ya sherehe za kunywa pombe zilizofanyika katika afisi na makazi yake ya Downing Street kipindi nchi ilipokuwa imefungwa, ameliambia bunge leo kwamba hatojiuzulu. 

Johnson ana wakati mgumu kutuliza hali hata ndani ya chama chake ambapo baadhi ya wabunge walioghadhabishwa na sherehe hizo wanamtaka aachie ngazi. 

Huku hayo yakiarifiwa, Waziri Mkuu huyo amesema kuwa watu nchini England hawatohitajika kuvaa barakoa mahali popote au kufanyia kazi nyumbani kuanzia wiki ijayo. 

Johnson amesema wanasayansi wanaamini kwamba wimbi la kirusi cha Omicron limesambaa kote nchini humo. 

Ameongeza kwamba hatua ya kuonyesha vyeti vya chanjo ya corona itafikia kikomo pia ingawa biashara zitaamua iwapo zitaendelea na utaratibu huo au la.


Post a Comment

0 Comments