Ticker

6/recent/ticker-posts

 


TCRA Watoa Tamko "Hakuna Tatizo Katika Mabadiliko ya Vifurushi Vinavyotumika Kwa Sasa"

 


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kuwa mabadiliko ya vifurushi vinavyotolewa hivi sasa na watoa huduma za mawasiliano nchini viko sahihi na wao wanavitambua.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mkuu wa TCRA Dkt, Jabiri Bakari amesema kuwa mamlaka imekuwa ikifuatilia kuhusu mabadiliko ya vifurushi na kubaini hakuna tatizo Katika huduma hiyo

Aidha amesema watoa huduma wamekuwa na vigezo katika kupanga bei za huduma za mawasiliano, ikiwemo data pamoja na gharama za uwekezaji na uendelezaji.

Post a Comment

0 Comments