https://monetag.com/?ref_id=TTIb Johnson Sakaja ndiye Gavana mpya wa Nairobi | Muungwana BLOG

Johnson Sakaja ndiye Gavana mpya wa Nairobi


John Sakaja ameibuka mshindi wa wadhfa wa ugavana wa mji mkuu wa Kenya Nairobi. Bwana Sakaja alimshinda mwenzake wa chama cha Jubilee kutoka Muungano wa Azimio Polycarp Igathe baada ya kujipatia kura 699,392. Bwana Igathe alijipatia kura 573, 516.


Edwin Sifuna kutoka chama cha ODM alijipatia kura 716,876 na kuidhinishwa kuwa seneta wa jiji la Nairobi baada ya kumshinda mwenzake wa UDA Margeret Wanjiru. Wanjiri alijipatia kura 524,091.


Kwa upande wa Mwakilishi wa wanawake katika Jiji la Nairobi, mgombea wa chama cha ODM Esther Passaris (ODM) alijipatia kura 698,929dhidi ya mpinzani wake wa karibu Millicent Omanga wa UDA, ambaye alijipatia kura 586,246.


Post a Comment

0 Comments