Michuano ya ngoma za asili kivutio UMISSETA 2022


Michezo ya ngoma za asili ni miongoni mwa vivutio katika   Mashindano ya michezo kwa  Shule za Sekondari (UMISSETA)  yanayoendelea kufanyika  Mkoani Tabora.


 Agosti 13, 2022 washiriki wameonesha umahiri wa kucheza ngoma za asili kutoka katika Mikoa yao pamoja na ngoma za asili kutoka Mikoa  nje ya Mikoa yao.

Mkoa wa Arusha ndio uliofungua jukwaa kwa kuonesha ngoma za asili ya Mkoa huo unaohusisha makabila ya wamasai, wameru na wa Arusha, huku  Washiriki wa Mkoa wa Kagera wakicheza kwa madaha ngoma ya kabila la Kihaya.

Kwa  upande wa Mkoa wa Dodoma, washiriki walicheza ngoma ya kabila la wagogo ambayo huchezwa katika shughuli mbalimbali ikiwemo wakati wa mavuno na sherehe.

Washiriki wa  Mkoa wa Dar es Salaam  nao hawakuwa nyuma kwani walionesha mbwembwe zao kwa kucheza ngoma ya kabila la wazaramo.

Mkoa wa Singida ulionesha umahiri kupitia ngoma ya kabila la wanyiramba wanaopatikana Wilaya ya Iramba huku Tanga ikicheza ngoma ya kabila la Wazigua wanaopatikana wilaya ya Handeni.

Post a Comment

0 Comments