https://monetag.com/?ref_id=TTIb Ukraine yatoa wito wa vikwazo zaidi kwa Urusi | Muungwana BLOG

Ukraine yatoa wito wa vikwazo zaidi kwa Urusi


Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amezitolea wito nchi za Magharibi kuweka vikwazo dhidi ya sekta ya nyuklia ya Urusi, kufuatia mgogoro unaokihusu kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya. 


Katika hotuba yake kwa njia ya video, Zelensky amesema Urusi inatumia kinu cha nyuklia hicho kilichopo kusini mwa Ukraine kuwatisha watu, kuusaliti uongozi wa Ukraine na dunia nzima.Kiev na Moscow zimekuwa zikishutumiana kwa siku nyingi kuhusika katika uvamizi wa kinu hicho kikubwa kabisa cha nguvu za nyuklia barani Ulaya.


Zelensky alionya kwamba kupelekwa kwa vikosi vya Urusi kwenye eneo la mtambo huo wa nyuklia kunaongeza tishio la mionzi kwa Ulaya kufikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa hata katika nyakati ngumu zaidi za mapambano ya Vita Baridi.Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mnamo Februari kumeshuhudiwa uhalifu mkubwa dhidi ya raia, ambao Kiev na jamii ya kimataifa zinailaumu Moscow.

Post a Comment

0 Comments