https://monetag.com/?ref_id=TTIb Vyombo vya moto nchini kuanza kukaguliwa | Muungwana BLOG

Vyombo vya moto nchini kuanza kukaguliwa


Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani linatarajiwa kuanza ukaguzi wa vyombo vyote vya moto nchini yakiwemo magari binafsi, magari ya usafirishaji, bajaji na hata pikipiki, ambapo mara baada ya ukaguzi yatapatiwa stika maalumu za ukaguzi.


Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Ramadhani Ng'anzi, wakati akizungumza hii leo Februari 6, 2023, jijini Dar es Salaam, na kueleza mbali na hatua hiyo pia wamewasilisha maombi ya marekebisho ya kanuni za usafirishaji kwa mabasi ya kukodi kuwa na ukomo wa kusafiri nyakati za usiku.


Kamanda Ng'anzi amesema Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani linaendelea na uchunguzi wa tukio la ajali lililohusisha kugongana kwa magari mawili lililotokea eneo la Korogwe na kusababisha vifo vya watu 20 na wengine wakijeruhiwa.


Wakati hayo yakijiri, hii leo Bungeni jijini Dodoma Mwenyekiti wa Kamati ya Kumudu  ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vita Kawawa, wakati anawasilisha taarifa yake amesema kwa kipindi cha mwezi Oktoba-Desemba 2022 matukio ya ajali yaliyosababisha vifo katika kipindi hicho ni 281 ikilingwanishwa na  matukio 273 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la makosa 8 sawa na asilimia 2.9.

Post a Comment

0 Comments