https://monetag.com/?ref_id=TTIb Waliochapisha habari kuhusu vijana 147 wa JKT kuwa na VVU watakiwa kuomba radhi na kuzifuta | Muungwana BLOG

Waliochapisha habari kuhusu vijana 147 wa JKT kuwa na VVU watakiwa kuomba radhi na kuzifuta


Jeshi la kujenga Taifa (JKT) limevitaka vyombo vyote vya habari na Mitandao ya Kijamii kuomba radhi na kuondoa mara moja picha za Vijana 147 wa jeshi hilo kuwa na maambikizi ya (VVU) ambapo vilitoa habari hiyo kwa kuweka picha za vijana wa JKT ambao sio wahusika wa habari hiyo.


Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Tawi la Utawala (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena wakati wa Kikao na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma na kusema kitendo hicho ni Udhalilishaji wa Utu wa mwanadamu na ukosefu wa Maadili ya Uandishi wa Habari.

Aidha amesema Jeshi la JKT limefafanua kuwa kabla ya kuanza Mafunzo ya Jeshi hilo Vijana wanaojiunga hufanyiwa usahili wa nyaraka zao ikiwemo vipimo vya Afya ili kufahamu Utimamu wa Mwili ili kubaini changamoto za kiafya walizonazo.

Katika Hatua nyingine ameongeza kuwa kigezo cha Afya kwa Vijana wanaokuja Kambini endapo wamebainika kuwa na changamoto za kiafya kinazingatiwa kwa kuwekwa chini ya Uangalizi Maalum.

Jeshi la Kujenga Taifa linapenda kuutarifu Umma kuwa Mafunzo ya Jeshi hilo ni Salama yenye kuzingatia Sheria na taratibu za Miongozo ya Malezi ya Vijana wanapopelekwa makambini wanalelewa vizuri kulingana na Mila na Desturi za Nchi yetu.

Post a Comment

0 Comments