SIKU chache baada ya kushinda kesi ya tuhuma za kubaka
iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam , mwimbaji wa
muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha anatarajiwa kupandishwa tena katika korti
hiyohiyo kwa madai mengine, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
Mwimbaji wa muziki wa
Injili, Emmanuel Mbasha.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni kwa sharti la
kutotajwa jina, mmoja wa watu wa karibu na wanandoa hao, alisema Flora
amefungua kesi ya madai ya talaka katika Mahakama ya Kisutu na kwamba muda si
mrefu shauri hilo
litaanza kusikilizwa.
“Flora ameenda
mahakamani kudai talaka yake, kwa hiyo kesi inatarajiwa kuanza kusikilizwa muda
wowote kuanzia sasa,” alisema mtoa habari huyo.Baada ya taarifa hizo, mwandishi
wetu alimtafuta Mbasha kwa njia ya simu na kumuuliza juu ya madai hayo, ambapo
alikiri na kudai anajiandaa kukabiliana na shitaka hilo .
“Yeah, ni kweli kaka,
Flora ameamua kwenda mahakamani kudai talaka yake, sioni kama
ni tatizo, kwa sasa siwezi kuzungumza lolote kwa sababu limeshafika katika
mkondo wa sheria na tunapaswa kusubiri tuone kitakachotokea, lakini naamini
kila kitu kitakwenda sawa,” alisema Mbasha.
Kwa upande wake, mke wa mwimbaji huyo, ambaye pia ni mkali
wa nyimbo za gospo, Flora Mbasha alipotafutwa hakupokea simu yake ya mkononi,
lakini alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) alijibu kwa kifupi:
“Kaka, naendesha,
kila kitu kiko mahakamani kwa hiyo sina la kuzungumza kwa sasa.”
Hali hiyo inatokea siku chache tu baada ya mahakama hiyo
kumuachia huru mwimbaji huyo aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya ubakaji
ambayo pia yalimleta mkewe huyo mahakamani akiwa shahidi wa upande wa mashtaka.
Kwa muda mrefu, waimbaji hao wamekuwa katika mgogoro wa
kifamilia ambapo juhudi za watu mbalimbali zimefanyika kusuluhisha lakini
hazikufanikiwa.