JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DARE SALAAM LAVUNJA KAMBI YA KIKUNDI KINACHODAIWA KUENDESHA UGAIDI WA KIHALIFUJESHI la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam limevunja kambi inayodaiwa kuendesha uhalifu wa kigaidi wa kuvamia vituo vya polisi na kunyanganya silaha kwa ajili ya kuendeleza uhalifu na kuweza kukamata watuhumiwa saba.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema kundi limenaswa kutokana na taarifa mbalimbali  k mauaji ya kinyama na uporaji silaha.

Amesema kundi hilo linalodaiwa kuendeshwa na familia moja ya Ulatule limekuwa likiendesha matukio mengi ya uhalifu  ya kupora silaha  katika vituo vya polisi.

 Majambazi hao walikamatwa wakiwa na bunduki nne  pamoja na risasi 18 aliwataja majina watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Mohamed Ulatule (67) ‘Uso a wa Simba’ , Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga mkoa wa Pwani,Ramadhan Ngande (29)Miaka 29, Dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Kongowe,Hamis Ulatule (51),Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani,Alli Ulatule(65), Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani,Nassoro Ulatule  (40), Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani,Seleman Ulatule (83),Mkazi wa Mamdimkongo, Said Chambeta (40) ‘Mzee wa Fasta’Mfanyabiashara wa Mitumba, Mkazi wa Yombo Makangarawe kati yao Mtuhumiwa wanne ni wa familia moja inayojihusisha na vitendo vya ujambazi pamoja na  vya kigaidi.

 Wakati huo Jeshi la Kanda Maalum ya Dar es Salaam,limewakamata watuhumiwa sita wa mauaji wa Askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu Morogoro,Elibariki Pallangyo lilolofanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es Salaam.

 Kova amesema katika tukio la kukamata watu hao kiongozi wao, Omary Salehe (Bonge Mzito) alisema kuna silaha ikiwa ni njia ya kutaka kutoroka katika mikono ya polisi ambapo polisi walitumia mafunzo yao vizuri na kufanikisha kumjeruhi na alifariki wakati akipelekwa Hospitali.

 Wengine ni Said Mazinge (37) Mkazi wa Tegeta Kibaoni
 Rashid Watson  (21)‘Dodo’Mkazi wa  Vingunguti, Ramadhan Salum (38)’Nguzo Mkazi wa Mbagala Kiburugwa  Bakari Rashidi  (38) ‘Malenda’  Mkazi wa Mbagala kizuiani Hamis Hamis (24) ‘Freemason  Mkazi wa Mbezi .