Agizo la Dk Magufuli latekelezwa Magereza

Dar es Salaam. Agizo la Rais John Magufuli la kutaka wafungwa watumike kwenye uzalishaji mali, limeanza kutelekezwa na Jeshi la Magereza katika ujenzi wa nyumba 320 za maofisa na askari wake.

Akiwa wilayani Bagamoyo, Septemba 30 kufunga mafunzo ya medani za kijeshi, Rais Magufuli aliitaka Magereza kuanza kuwatumia wafungwa katika shughuli zake.

Magereza wameanza kutekeleza agizo hilo katika ujenzi wa nyumba hizo zitakazojengwa kwenye Gereza la Ukonga na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Ujenzi wa nyumba hizo umeanza baada ya kupita siku 26 tangu Rais Magufuli alipotembelea gereza hilo kisha kuahidi kutoa Sh10 bilioni za ujenzi huo.
Mpya zaidi Nzee zaidi