Dar es Salaam. Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa amewataka wakristu wote nchini kutumia vipaji na karama walizojaaliwa kuwahudumia na kuwainua watu wengine.
Akizungumza wakati wa Ibada ya Misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini hapa usiku huu, Askofu Nzigilwa amesema Mungu amemjalia kila mtu kipaji chake, kwa hiyo ni vema akakitumia kuwainua wengine.
Amesema binadamu ameumbwa kwa upekee, hivyo asikubali ubinadamu wake uchezewe na wengine.
Amesisitiza juu ya utii kwa Mungu na kwa binadamu wote, mkubwa kwa mdogo.
“Utii ni jambo muhimu katika maisha yetu na siyo udhaifu kama wengine wanavyodhani. Watoto wawatii na kuwaheshimu wazazi wao,” amesema.
Askofu huyo amesisitiza juu ya upatanisho kama njia ya kumaliza migogoro katika jamii.
Amesema kila mtu akiwa mpatanishi hakutakuwa na migongano katika jamii.