Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amesema changamoto kubwa aliyokumbana nayo wakati wa uongozi ilikuwa ni ununuzi wa vifaa vya uchaguzi mwaka jana.
Alisema uchaguzi huo ndiyo uliokuwa na ushindani mkubwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, hivyo ilikuwa ni lazima vifaa vya kisasa viwapo zikiwamo mashine za BVR ambazo zilitumika kwa mara ya kwanza.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Jaji Lubuva alisema kulikuwa na tatizo la upatikanaji wa fedha za ununuzi wa mashine hizo ikiwa imebaki miezi michache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
Hata hivyo, alisema walifanikiwa kununua vifaa hivyo na kuvitumia kwenye uchaguzi huo.
“Tumeweka misingi katika Tume ya Uchaguzi, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mashine za BVR na kuongeza uwazi kwenye uendeshaji wa chaguzi zetu. Wananchi wawe na imani na tume, namfahamu mwenyekiti mpya (Jaji Semistocles Kaijage) najua atafanya kazi nzuri,” alisema.
Jaji Lubuva aliongeza kuwa changamoto nyingine zilikuwa za kawaida na hazikumsumbua.
Mwenyekiti huyo mstaafu wa NEC alisema alipata ushirikiano kwa wafanyakazi wa tume hiyo na kwamba ana imani mwenyekiti mpya ataendeleza pale alipoishia.
Pia, aliwataka wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu ameiacha tume hiyo kwenye mikono salama, na kwamba Jaji Kaijage ni mtu makini mwenye uwezo wa kuisimamia kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Septemba 13 2015, vifaa vya uchaguzi vyenye thamani ya Sh41.6 bilioni viliwasili nchini na kuanza kusambazwa kwenye mikoa mbalimbali.
Hata hivyo, karatasi za kupigia kura zilichelewa na kuwasili mwishoni mwa mwezi huo.
Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa NEC, Eliud Njaila alieleza kwamba kufikia huo tume ilikuwa imepokea vifaa 70,000.
Alisema baadhi ya vifaa vilitengenezwa na wazabuni wa ndani na vingine kutoka nje.
Vifaa vya uchaguzi vilivyonunuliwa vilikuwa ni pamoja na vibanda vya kupigia kura (vituturi), taa za kumulikia wakati wa kuhesabu kura, mihuri, vitabu vya maelekezo kwa wapigakura na masanduku.