Dar es salaam. Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema amani ya kweli katika nchi itapatikana kwa kuwajali masikini.
Akitoa mahubiri katika Misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa Kuu la Mt. Joseph jijini Dar es Salaam usiku huu, Kardinali Pengo amesema Yesu Kristo alizaliwa katika hali ya umasikini ili kuleta tumaini na amani kwao kabla ya matajiri.
“Hatuwezi kujua kwa nini Mwana wa Mungu alizaliwa katika zizi la ng’ombe na alizaliwa kwa watu masikini na kutangaza kwao habari njema. Mara nyingi tunadhani inapatikana kwa wenye uwezo wa kifedha. Tunapotafuta amani tusiwategemee hao, bali masikini ambao walipelekewa ujumbe,” amesema Pengo.
Hata hivyo, Kardinali Pengo ameonya kuwapo kwa masikini wenye hamu ya kuwa matajiri akisema wanaweza kuhatarisha amani.
“Masikini mwenye hamu ya kutajirika ni hatari kuliko tajiri. Kila mtu atekeleze wajibu wake ndipo awe chimbuko la amani. Tunapodai amani tuwe wa kwanza kuwa mfano,” amesema Kardinali Pengo.