Dar es Salaam. Kusimama kwa moyo ghafla ndicho chanzo cha kifo cha chipukizi wa Mbao FC ya Mwanza, Ismail Halfan Mrisho.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi wakati akizungumzia chanzo cha kifo cha mchezaji huyo kilichotokea Jumapili wakati akiitumikia timu yake katika Ligi ya Vijana dhidi ya Mwadui uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Jumapili.
“Daktari amesema tatizo ni kusimama kwa moyo kwa hiyo sina nyongeza, marehemu hakuwa na jeraha lolote hiyo ndiyo taarifa,” alisema Kamanda Ollomi akimnuku taarifa ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa mkoa huo, Dk. Thomas Rutta.
Hata hivyo, kuna mambo yaliyojitokeza, yanayohitaji uelewa ili kuwasaidia wanamichezo na watu wengine nchini.
Kwanza, ni sababu za vifo vya ghafla kama cha kijana huyo wa Mbao FC na pili, namna ya kuwasaidia wanaokumbwa na matatizo kama hayo.
Kwa kawaida, mwanamichezo hufanya mazoezi yanayoulazimisha moyo kufanya kazi kubwa ya kusukuma damu nyingi inayohitajika na misuli ili kufanya vitendo mbalimbali wakati akicheza.
Inapotokea tatizo lolote la kiafya katika moyo, inaweza kuchochea kuanguka ghafla na hatimaye kupoteza maisha.
Kwa kawaida, matatizo ya moyo hujificha, huwa kimya mwilini na yanaweza yasigundulike hata wakati wa wanamichezo wanapofanyiwa uchunguzi wa kina wanapoanza kucheza au kujiunga na klabu.
Ni kawaida kusikia maneno kama shambulizi la ghafla la moyo, moyo kushindwa kufanya kazi.
Huduma inayojulikana kitaalamu, Cardio Pulmonary Resurcitation au CPR inatajwa na madaktari, kipindi hiki cha tukio la kifo Ismail aliyeanguka ghafla na kufia uwanjani.
Kitabibu, ‘heart attack’ ina maana ni pale mishipa ya damu inayopeleka damu safi katika moyo ijulikanayo kama coronary artery inapokuwa na kizuizi.
Mishipa hiyo inaweza kuharibika na kuwa miembamba au ikazibwa na vichuguu vilivyokuwa katika kuta zake au kuzibwa na mabonge ya damu yaliyoganda.
Hali hiyo husababisha misuli ya moyo kukosa damu na hivyo kufa.
Kwa kifupi, shambulizi la moyo ni kufa/kuoza kwa sehemu ya misuli ya moyo (myocardial infaction). Hali hii ni tatizo linalosababisha moyo kushindwa kufanya kazi.
Cardiac arrest, yaani kusimama kwa mapigo ya moyo hutokea pale mapigo ya moyo yanapodunda bila mpangilio na kwenda mrama, hali hii hujulikana kitabibu kama ventricular fibrillation.
Hali hiyo inatokea wakati mtiririko wa umeme wa moyo unapopata hitilafu ya ghafla. Kwa kuwa umeme wa moyo ndiyo unaoratibu kutokea kwa mapigo ya moyo pale kunapokuwa na hitilafu husababisha kusimama ghafla.
Hali hii ndiyo huwa na matokeo ya kusimama ghafla kwa mapigo ya moyo na kusababisha vifo vya ghafla. Pamoja ya kwamba tatizo hilo ni tishio kwa kusababisha vifo vya ghafla linaweza kudhibitiwa kama mgonjwa atawahi kupata huduma ya kwanza, Cardio Pulmonary Resuscitation (CPR).
Huduma hii ni moja ya huduma za dharura anazopewa aliyeanguka ghafla. Ndani ya huduma hii kuna huduma ijulikanayo kama utomasaji wa moyo (cardiac massage) na utoaji wa hewa ya oksijeni.
Huduma hii ndiyo aliyotakiwa kupewa mchezaji aliyeanguka ghafla uwanjani, pengine ni kukosekana kwa wataalamu wa afya uwanjani au wananchi wa kawaida wenye ufahamu wa huduma za msingi wa utomasaji wa moyo.
CPR inaweza kutolewa katika eneo lilipotokea tukio na katika huduma za afya katika idara ya huduma za dharura. Huduma hii inahitajika kufanyika haraka iwezekanavyo kwa mgonjwa ambaye amepoteza fahamu au aliyeanguka ghafla au kutulia.
Huduma hii inaweza kutolewa kwa mtindo wa aina mbili. Hufanywa na mtu mmoja au watu wawili. Lengo kuu la huduma hii ni kumsaidia mtu mwili wake upate oksijeni katika moyo na ubongo.
Kutimia kwa lengo hili ni lazima kusaidia mfumo wa hewa kufanya kazi kwa kusukuma hewa kuingia puani na utomasaji wa moyo kwa mtindo wa ugandamizaji wa kifua ili kusaidia mapigo ya moyo kudunda.
Panapokuwa na uwezekano huduma hii huenda sanjari na kutolewa kwa mawimbi maalumu ya umeme yanayotolewa na kifaa tiba maalumu kijulikanacho kama defibrillator.
Kifaa hiki huwekwa kifuani kwa mgonjwa, upande ulipo moyo na kinapowashwa hutoa mawimbi ya umeme ambayo husaidia kurekebisha hitilafu za chaji za umeme wa moyo.
Pengine ingeliwezekana kuokoa maisha ya chipukizi Ismail endapo kungekuwapo uwanjani na watoa huduma ya kwanza wenye ujuzi huo pamoja na defibrillator, ambayo ni rahisi kubebwa.
Kwa nchi zilizoendelea, ufahamu wa huduma hii unatolewa kuanzia elimu ya awali, wanapewa ujuzi na wanaweza kutoa msaada inapotokea matukio ya watu kuanguka na kupoteza fahamu.
Wasiwasi watanda Mbao FC
Baadhi ya wachezaji wa Mbao FC waliokuwa na Ismail mkoani Kagera kabla ya kifo chake walieleza kuwa kimewaacha na wasiwasi.
Mchezaji Ibrahim Hashim alisema kabla ya mwenzao kupoteza maisha alikuwa vizuri tangu wafike Kagera na kwamba hakuonyesha dalili za kudhoofika.
“Hali yake ilikuwa nzuri, tulikuwa na furaha sote tukisema kwamba tukifunga ni kushangilia kistaili, tunacheka lakini tulishangaa ile kuanguka na kufa ghafla, ” alisema Hashim.
Baba mzazi ashindwa kuongea
Baba mzazi wa Ismail, Khalfan Mrisho alishindwa kuzungumza kifo hicho, huku akionekana kutokwa machozi mfululizo.
RC Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela aliyeshiriki maziko hayo juzi alisimulia namna alivyoguswa na kifo hicho, akisema Taifa limepoteza kijana ambaye angeifikisha mbali nchi katika soka.
Alisema kuwa licha ya kutomfahamu kwa sura, lakini historia inaonyesha namna gani kijana huyo alivyokuwa akitegemewa kwa baadaye. “Ni msiba mkubwa, kila mmoja umemgusa, binafsi nilikuwa simjui, lakini historia niliyosikia kijana huyo alikuwa anategemewa na Taifa, tumuombee alazwe mahali pema peponi,” alisema Mongella, akimuita Ismail ‘Samatta mpya’.
Kauli ya TFF
Mwakilishi kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF), Yahya Hamad, ambaye ni mwenyekiti wa Bodi ya Ligi alisema Taifa limempoteza Samata mwingine, ambaye angeing’arisha nchi kwa baadaye.
MZFA walonga
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA), Jackson Songora alisema pigo hilo litakuwa historia kubwa kwa mkoa huo.
Alisema kama uongozi wa MZFA umepokea kwa maumivu makubwa kifo cha kinda huyo, aliyezikwa juzi ambaye pengine walimtarajia kuutangaza mkoa wao.
Viongozi wa dini
Shekh wa msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza, Hamza Mansoor alisema kuwa kifo hicho kwa kijana huyo ni pigo na kuwaomba wanafamilia kuwa wavulivu kwa kipindi hiki.
Pia, sheikh huyo aliwataka wananchi kujikita kwenye matendo mema na kuacha kuitumikia dunia na kusahau akhera (mbinguni).
Mchezaji huyo alikumbwa na mauti Jumapili iliyopita wakati timu yake ikicheza na Mwadui kwenye mashindao ya vijana chini ya miaka 20. Aliifungia timu hiyo bao kwenye ushindi wa mabao 2-0. Alizikwa juzi kwenye makaburi ya Mlango mmoja, Mwanza.
*Nyongeza na Saddam Sadick, Mwanza