F Mashauzi Kuachia Kiss Me Desemba Hii | Muungwana BLOG

Mashauzi Kuachia Kiss Me Desemba Hii

Mwanamuziki wa muziki wa taarabu hapa nchini Aisha Ramadhani (Isha Mashauzi) anataraji kuachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Kiss Me.

Akizungumza na globu ya jamii Msahauzi amesema kuwa amekuwa kimya kwa kipindi kirefu hivyo kibao hicho kitaweza kuwarudisha mashabiki wake katika mstari.

“hii ni zawadi ya kufunga na kufungua mwaka kwa mashabiki wangu hivyo wajue kuwa wimbo huo ambao upo katika viwango vya hali ya juu,imerekodiwa ndani ya studio za Sophia zilizopo kinondoni” amesema Mashauzi

Ameongeza kuwa waliniona kuwa nimekuwa kimya katika taarabu sasa nimerudi tena na hichi kibao ambacho watafurahi wenyewe.