F Polisi yafanyia kazi kauli ya Mzee wa Upako, kila kitu kujulikana leo | Muungwana BLOG

Polisi yafanyia kazi kauli ya Mzee wa Upako, kila kitu kujulikana leo

Tokeo la picha la mzee wqa upako

Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro 


Kauli ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki  tatu mfululizo akijibu yaliyoandikwa na vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani yake.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatoa ufafanuzi leo.