Tunaweza kusema kuwa Sikukuu ya Krismasi ya mwaka huu wa 2016 kwa nchini Tanzania imetolewa maalum kwa wakulima kutokana na ujumbe uliotolewa na viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya siku hii ukiwemo ujumbe kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli.
Ujumbe huo unatokana na tishio la Tanzania kukumbwa na ukame, ambapo wakulima kote nchi wametakiwa kuzitumia vizuri mvua zilizoanza kunyesha meneo mbalimbali ili kuzalisha mazao ya muda mfupi.
Akiwa ameambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli, Rais Magufu ameshiriki Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida na kuwaasa wakulima kote nchini kuzitumia vizuri mvua za sasa katika kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote pamoja na kulima mazao yanayostahimili ukame.
Amesema Sikukuu ya Krismasi kunadhihirisha kauli mbiu ya 'hapa kazi tu', kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa fundi mzuri wa useremala hivyo kuwataka watanzania kumuiga, na pia akiwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao la alzeti ili kuviwezesha viwanda vya kukamua mafuta ya alzeti kupata mbegu nyingi.
Awali Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Edward Mapunda, amewakumbusha wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanatunza mazingira ili yaweze kuwatunza na kuwaepusha na ukame wa mvua.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mustafa Kijuu aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye ibada ya Krismasi kitaifa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mwokozi Usharika wa Bukoba Mjini, amekiri kuwepo kwa upungufu wa chakula mkoani humo huku akitaja sababu kuu kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha ukame mkoani humo.
Kijuu amesema kwa sasa hali imeanza kukaa vizuri kutokana na mvua zilizoanza kunyesha na kuwataka wakulima kulima mazao yanayostahimili ukame, pamoja na mazao ya muda mfupi kama vile viazi na mihogo.
Ujumbe huo unatokana na tishio la Tanzania kukumbwa na ukame, ambapo wakulima kote nchi wametakiwa kuzitumia vizuri mvua zilizoanza kunyesha meneo mbalimbali ili kuzalisha mazao ya muda mfupi.
Akiwa ameambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli, Rais Magufu ameshiriki Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida na kuwaasa wakulima kote nchini kuzitumia vizuri mvua za sasa katika kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote pamoja na kulima mazao yanayostahimili ukame.
Rais Magufuli na Mkewe katika ibada ya Krismasi.