Zana haramu za Uvuvi zenye Thamani ya milion 15 zakamatwa na kuchomwa Wilaya ya Momba

Wilaya ya Momba yafanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu za uvuvi  katika Ziwa Rukwa.
Wilaya ya Momba Mkoani Songwe imefanikiwa kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya Sh 15,108,000/= zilizokamatwa ziwani Rukwa katika doria iliyofanyika tarehe 25 – 26/11/2016.
Zoezi hilo la utekelezaji  lililofanyika katika viwanja vya ofisi za kituo cha kilimo katika kata ya Kamsamba liliongozwa na Mkuu wa wilaya wa wilaya hiyo Mheshimiwa Juma Said Irando akiongozana na mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri hiyo, Adrian Jungu.

Awali akisoma taarifa ya mafanikio juu ya doria hiyo kwa mkuu wa wilaya, afisa uvuvi wa halmashauri hiyo bwana Pasco Kashinde alimwambia mkuu wa wilaya kuwa katika doria hiyo iliyofanyika kati ya tarehe 25 na 26/11/2016 walifanikiwa kukamata jumla ya makokoro 9 yenye thamani ya Sh 9,180,000/= na mengine 13 yenye thamani ya Shilingi 5,928,000/= yalisimamishwa kufuatia tangazo lililotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Momba tarehe 20/11/2016 lililowataka wavivu wenye nyavu haramu kusalimisha nyavu zao, hivyo makororo 22 yenye thamani ya Shilingi 15,108,000/= yatateketezwa siku hiyo na mkuu wa wilaya na kufanya jumla ya makorokoro 168 yenye thamani  ya Shilingi 131,864,000/= yawe yameteketezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2007.

Akiongolea hali ya ziwa hilo afisa uvuvi huyo alimueleza Dc Irando kuwa Ziwa Rukwa linakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazigira kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha ziwa kujaa tope na kina chake kuzidi kupungua mwaka na kutaka juhudi za maksudi kuchukuliwa ili kuweza kunusuru ziwa hili.

Afisa uvuvi huyo alimueleza mkuu wa wilaya kuwa pamoja na mafanikio katika doria hiyo lakini halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuharibika kwa boti yao ya Doria.

Naye Dc Irando akiongea mara baada ya utekelezaji wa zoezi hilo alimuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kutenga fedha katika bajeti ijayo kwa ajili ya ununuzi wa boti mpya na ya kisasa ili kukabiliana matumizi ya zana haramu na uharibifu wa mazingira katika ziwa hilo pia Irando alilisitiza kuwa doria hiyo ni endelevu na kuwataka wavuvi wanaoendelea kutumia zana haramu kujisalimisha kabla sheria kuchukua mkondo wake na kuwataka wananchi wanaoishi jirani na ziwa hilo kuacha kufanya shughuli za uzalishaji mali kando kando ya ziwa hilo kwani ni makosa kisheria.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha halmashauri ya Kamsamba Joseph Elias Mfukwe, amesema kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa samaki katika ziwa Rukwa kutoka na matumizi ya zana haramu nayayopelekea uharibifu wa mazingira ya samaki kuzaliana na wao kama serikali kwa sasa wanatoa elimu kwa wavuvi juu ya upungufu huo na matumizi ya zana haramu na kuwataka wavuvi wanaovua katika ziwa hilio kuacha matumizi ya zana haramu.

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kamsamba na vijiji jirani waliohudhuria uteketezaji huo wa zana haramu waliipongeza Serikali kwa juhudi walizochukua na kukamata zana hizo na kuitaka Serikali kuongeza juhudi zaidi ili kukabiliana na matumizi ya zana hizo pampoja na kuwakamata wavuvi wenyewe pamoja na zana hizo pia wanavijiji hao walimueleza mkuu wa wilaya kuwa kwa sasa wavuvi  hao wamekimbilia katikati ya ziwa wakitumia milipuko na dhana nyingine haramu kuvua samaki na kumuomba mkuu wa wilaya kulifanyia kazi suala hilo.

Akijibu ombi la wananchi hao Dc Irando alisema amelipokea na ataviagiza vyombo vyake vya ulinzi kuendesha doria nyingine ziwani humo na kuwaomba wananchi hao kushirikiana na Serikali kukabiliana na uvuvi huo harama.

Kiutawala ziwa Rukwa linamilikiwa na Mikoa ya Songwe, Rukwa, Katavi na Tabora, katika mkoa wa Songwe ziwa Rukwa linapatikana Kaskazini mwa makao makuu ya wilaya ya Momba na lina kilometa za Mraba 1,010 ambapo ziwa hili katika Wilaya ya Momba lina ukubwa wa kilometa za mraba 292 sawa na asilimia 28.91 ya ukubwa wa ziwa lote likiwa na vyombo vya uvuvi 254, wavuvi  532 vyombo vye injini 4 na visivyo na injini 250.



Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia