Ajali ya Treni: 30 wapioteza maisha, wengine bado wamenaswa

Ajali ya Treni IndiaTakriban watu thelathini wamepoteza maisha yao nchini India baada ya Treni waliyokuwa wamepanda kuacha reli na kuvamia upande wa pili.

Hii ilitokea wakati wa safari kati ya Jagdalpur na Bhubaneswar katika jimbo la Andra Pradesh usiku wa Jumamosi.

Ripoti zinasema watu wengi bado wamenaswa ndani ya Treni hiyo na huenda kwasababu hiyo idadi ya waliofariki ikaongezeaka.

Mpaka sasa watu hamsini ndio walioripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo.

Ajali ya Treni hutokea mara kwa mara nchini India kutokana na miundo mbinu duni na kuchakaa kwa reli.

Mnamo mwaka jana zaidi ya watu mia moja na arobaini walifariki kutokana na ajali kama hii kaskazini mwa jimbo la Uttar Pradesh.

Hata hivyo maafisa wa uokozi wanaendelea kuonyesha juhudi katika kuwafikia manusura wa ajali hiyo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items