Alichikisema Mzee Mwinyi kuhusu Wananchi wanapokosa haki zao mahakamani


Tabia iliyokithiri ya wananchi kutoridhika na maamuzi ya mahakama na kuamua kwenda kupata suluhu ya matatizo yao katika ofisi za wakuu wa mikoa au wilaya ndio chanzo kikubwa cha wananchi hao kukosa haki yao ya kisheria kutokana na njia hiyo kuwa ndefu na isiyowaletea maamuzi yanayotakiwa na kujikuta wakipoteza muda ambao wangekata rufaa.

Kauli hiyo imetolewa na rais mstaafu wa awamu ya pili,ALHAJI ALI HASSAN MWINYI,wakati alipokuwa anazindua wiki ya sheria hapa nchini baada ya kufanya maandamano yaliyoshirikisha kaimu jaji mkuu,majaji wa mahakama kuu,wansheria na vikundi vya jamii kutoka wilaya zote tatu za jijini DAR ES SALAAM,na kusomwa kwa niaba yake na msaidizi wake.

Amesema tabia hiyo aliiyona alipokuwa rais wa nchi hii miaka ya themanini na siku zote alikuwa akiwapa ushauri waliokuwa wakilalamika kuwa wakakate rufaa mahakama ya rufaa ili waweze kusikilizwa kesi zao na hatimae waweze kupata haki waliokuwa wanaitafuta.

Kwa upande wake kaimu jaji mkuu wa TANZANIA,PROFESSA JUMA KHAMISI,mwananchi kwa mujibu wa tafsiri ya ibara ya 8 ya katiba ambayo inasema mwanachi ndie mwenye mamlaka ya maisha na mihimili mitatu ya dola yaani bunge utawala na mahakama zipo kwa ajili ya kustawisha maisha ya mwananchi.

Wiki ya sheria hapa nchini itaadhimishwa kwa muda wa wiki moja kuanzia leo tarehe 29 mwezi huu hadi itakapofikia kilele ifikapo tarehe 8 ya mwezi february ambapo katika viwanja vya MNAZI MMOJA kutakuwa na maonesho yatakayojumuisha idara mbalimbali za mahakama,magereza,polisi,mkemia mkuu,Takukuru na uhamiaji ambapo watapokea maswali mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Mpya zaidi Nzee zaidi