Wikiendi iliyopita Arsenal wamepata ushindi zidi ya Burnley.Hadi dakika ya 90 ya mchezo huo ilionekana utaisha kwa sare ya goli moja kwa moja lakini katika dakika za majeruhi Arsenal walipata penati.Arsenal ambao walikuwa 10 uwanjani baada ya kiungo wao Granit Xhaka kutolewa nje kwa kadi nyekundu walifunga penati hiyo kupitia kwa Alexis Sanchez.
Haikuwa mara ya kwanza kwa Burnley kufungwa na Arsenal katika dakika za mwisho za mchezo.Kwani mwezi wa kumi mwaka jana Burnley walienda na Arsenal hadi dakika ya 90 wakiwa bila kwa bila lakini Laurent Kolcieny aliwafunga goli la dakika za mwisho kabisa wa mda wa majeruhi na Arsenal wakimaliza mchezo huo kwaushindi wagoli hilo.
Arsenal msimu huu dakika za mwisho za mchezo zimeonekana zikiwa upande wao.Manchester United nao mechi yao zidi ya Arsenal waliamini wataibuka ushindi wa bao moja lakini dakika ya tisini Olivier Giroud alisawazisha.Wameshafunga dakika hizo hizo za mwisho katika mchezo zidi ya Bournamouth Fc katika mchezo ulioisha kwa sare ya goli tatu kwa tatu huku Giroud akifunga goli la e dakika ya 92.
Magoli ya dakika hizo yamefungwa na Arsenal mara 12 katika msimu huu.Magoli hayo 18 yalifungwa baada ya dakika ya 80 ya mchezo.Hiini orodha ya timu zilizofunga magoli katika dakika za mwisho za mchezo msimu huu(baada ya dakika ya 80).
1.Arsenal (16)
2.Man City (15)
3.Chelsea (12)
4.Everton (12)
5.Crystal Palace (11)
6.Man United (10)
7.Totenham (10)
8.Sanswea (9)
9.Westham (9)
10.Bournermouth (8)
11.Liverpool (8)
12.Burnley (7)
13.Watford (6)
14.West Brom (6)
15.Southampton (6)
16.Leicester (6)
17.Sunderland (6)
18.Hull City (4)
19.Stoke City (3)
20.Middlersbrough (2)
