Chama Cha Mapinduzi -CCM katika kukabiliana na baadhi ya wanachama wanaopata uongozi kwa njia ya rushwa kimekuja na muundo utakaowezesha kupata viongozi waadilifu katika chaguzi za ndani za chama hicho zinazoanza mapema mwezi ujao kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa.
Akizungumza katika kongamano la maadhimisho ya miaka 40 ya chama hicho katibu mkuu mstaafu na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya ccm Wilson Mkama amesema chama cha mapinduzi kinatakiwa kupambana na adui rushwa nje ya mahakama.
Katibu mkuu huyo wa zamani wa Chama cha Mapinduzi amesema ili CCM iendelee kuwa imara inahitaji muundo utakaozalisha viongozi waadilifu pekee na kujiepusha wale wenye kukitia doa chama hicho.
Naye katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa mtwara Shaibu Akwilombe amesema sherehe hizo za miaka 40 ya CCM zitatumika kuhamasisha wanachama wake kutambua madhara ya rushwa hasa kipindi hiki cha kuelekea chaguzi za ndani za chama.
Mada kuu ya ngongamano hilo ni ccm mpya dhidi ya mapambano ya rushwa nje ya mahakama maalumu ya kifisadi.