Dkt. Mpango azindua jina na nembo mpya ya kibiashara ya benki ya posta tanzania (tpb bank plc)

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jina Jipya na Nembo Mpya yenye alama ya Kipepeo, (Tpb Bank Plc) vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania Plc, kuanzia Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Prof. Lettice Rutashobya na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiangalia Jina Jipya na Nembo Mpya iliyobuniwa na Benki hiyo baada ya kuizindua rasmi  Januari 19, 2017, Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wa pili kulia), akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, kwa kazi nzuri ambayo benki hiyo imefanya kubuni Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara ya Sekta ya Fedha kuanzia Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba kabla ya kuzindua rasmi Jina Jipya na Nembo vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), kuanzia  Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba ya mafanikio ambayo Benki yake imeyapata katika biashara ya Sekta ya Fedha ikiwemo kukuza mtaji, kupata faida na kufanikiwa kubuni Jina Jipya na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kutumika kuanzia leo Januari 19, 2017, baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

JIUNGE NASI 
 INSTA@MUUNGWANABLOG ,FB@MUUNGWANABLOG,YOUTUBE @MUUNGWANA TUBE, BOFYA HAPA KU-INSTALL APP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.
Mpya zaidi Nzee zaidi