Gereza aliko Mbunge Chadema lajulikana

Image result for lijualikali

MBUNGE wa Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Lijualikali, yupo katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela, imefahamika.
 
Jumatano iliyopita, Mahakama ya Wilaya ya Kilombero ilimhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila kulipa faini mbunge huyo kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, akizungumza na Nipashe jana kwa simu, alisema alimtembelea mbunge huyo kwenye Gereza la Ukonga alikofungwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Lissu ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, alisema mbunge huyo yuko vizuri kiafya na ameahidi kutorudi nyuma katika kupigania na kutetea haki za wananchi wa jimbo analiloliongoza.

JIUNGE NASI 
 INSTA@MUUNGWANABLOG ,FB@MUUNGWANABLOG,YOUTUBE @MUUNGWANA TUBE, BOFYA HAPA KU-INSTALL APP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.