WAKATI kuna wagonjwa 63 wa homa ya manjano waliokwishagundulika hadi kumalizika mwaka jana nchini Brazil, saba kati yao wamezaliwa nao, sasa serikali imeanza kuchukua hatua za ziada kuukabili.
Hadi sasa serikali inasema imeshatuma dozi milioni mbili za chanjo, huku Gavana wa jimbo ambalo limeathiriwa liitwalo Minas Gerais, ametangaza siku 180 au hali ya hatari.
Vifo vilivyotangazwa sasa, vinaelekezwa kuwa vingi zaidi kuliko vilivyowahi kutokea, tangu kusikika ugonjwa huu kwa mara ya kwanza mwaka 2008.
Hata kwa wakazi wa jimbo hilo, kinachofanyika sasa ni kwamba watu wanapewa chanjo walau kwa siku 10 kabla ya kusafiri kwenda jimbo lililoathiriwa.
Pia, katika jimbo la Sao Paulo, ambalo liko jirani na Minas ambako ndiko kumeathirika zaidi, nako wamebainika wagonjwa wanane.
Kitaifa bado haijagundulika namna maradhi hayo yalivyoingia mahali hapo na sasa yanasababisha magonjwa.
Shirika la Afya Duniani (WHO), limetoa ufafanuzi kwa watu kuuelewa ugonjwa huo. Iko kama ifuatavyo:
. Ni maradhi yanayosababishwa na virusi vinavyosambazwa na mbu kwenda kwa binadamu.
• Ugonjwa huo ni mgumu sana kuuchunguza na vigumu kuutofautisha na magonjwa mengine ya aina hiyo.
• Watu wengi hupata nafuu kila baada ya hatua ya kwanza ya kuathirika na kupata matibabu. Ni ugonjwa unaosababisha maumivu katika misuli, homa, maumivu ya kichwa na mgongo, mwili kutetemeka, kukosa hamu ya kula na kutapika.
• Kwa wastani wa asilimia 15 ya watu wanaougua kwa mara ya pili, hupatwa na homa kali, ngozi kuwa ya njano na figo kushindwa kufanya kazi.
• Wengi ambao sumu kali ya maradhi hayo yakiwaingia, huwa wanakufa ndani ya kipindi cha siku kati ya 10 na 14.
