
Waziri mkuu wa Israel aunga mkono mpongo wa ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico
Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu amuunga mkono rais wa Marekani Donald Trump kuhusu ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.
Waziri mkuu wa Israel aliyafahamisha hayo jana Jumamosi kuwa anaunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Trump kuhusu ujenzi wa ukuta mpakani mwa Marekani na Mexico.
Waziri Netanyahu alifahamisha kuwa ujenzi wa ukuta kusini mwa Israel ulifaulu kuzuia wahamiaji haramu nchini Israel.