JB awashangaa wasanii wanaolalamika kuhusu soko la filamu

Wakati wasanii wengi wa filamu nchini wakilalamika kuhusu soko la filamu kuwa baya huku wengine wakitishia kuachana na kazi hiyo kwa muda, Msanii mkongwe wa filamu nchini Jacob Steven ‘JB’ amedai tangu ameanza uigizaji hajawahi kupata changamoto ya soko la kazi zake kama ambavyo baadhi ya wasanii wa filamu bongo wamekuwa wakilalamika.


Kwa mujibu wa mtandao wa EATV, muigizaji huyo amedai hajawahi kupata changamoto hiyo na siku zote kazi zake zimekuwa zikifanya vizuri kila alipoingiza sokoni.

“Sijawahi kupata matatizo ya soko katika kazi zangu, kwa hiyo lazima niwe mkweli sijawahi kupata matatizo ya soko kazi zangu zimekuwa zikiuzwa na nilikuwa napata mauzo mazuri kwangu hivyo hilo lazima nimshukuru Mungu,” alisema JB.

Aliongeza, “Kizuri zaidi niliweza kutengeneza kazi ambazo mimi sikuigiza mimi ila zilifanya vizuri pia, labda mwaka 2003 wakati natoa kazi yangu ya kwanza kidogo lakini baada ya hapo nilipata mkataba wa kudumu, kwa hiyo mimi binafsi sijawahi kupata matatizo ya soko” alisema JB

Muigizaji huyo ambaye mpaka sasa ametengeneza filamu zaidi ya 40 ikiwa ni pamoja ya zile kazi alizoziandaa na kuigizwa na watu wengine. alidai mapema mwaka huu atatangaza kustaafu kuigiza ili abaki kama producer.

Mpya zaidi Nzee zaidi