Kichuya Afikisha Siku 78 Bila Ya Kufunga Bao Hata Moja, Sasa Ni Dakika 540

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amefikisha siku 78 bila ya kufunga hata mechi moja.

Mara ya mwisho, Kichuya aliifungia Simba kwa penalti ilipoivaa Stand United Novemba 2.

Lakini jana, Kichuya ameichezea Simba mechi ya sita ikiwa ni dakika ya 540 bila ya kufunga hata bao moja.


Kwa sasa Kichuya ana mabao tisa ya kufunga akiwa anaongoza msimamo wa wafungaji sawa na Simon Msuva na Amissi Tambwe anayshikilia tuzo ya mfungaji bora.

Mwanzoni mwa ligi, Kichuya ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar alionekana ni hatari huku akifunga mfululizo.

JIUNGE NASI 
 INSTA@MUUNGWANABLOG ,FB@MUUNGWANABLOG,YOUTUBE @MUUNGWANA TUBE, BOFYA HAPA KU-INSTALL APP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.
Mpya zaidi Nzee zaidi