Siku chache zilizopita Liverpool walitolewa katika mashindano ya EFL kwa kipigo cha goli moja dhidi ya Southampton.Baada ya kuondolewa katika FA jana tumeshuhudia tena Liverpool wakifungashwa virago katika michuano ya FA.
Sasa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kutokana na kipigo hicho hakuna mtu anayepaswa kuchukua lawama bali yeye.Jurgen Klopp amekubali zigo hilo la lawama kulibeba na sio wachezaji wake.
Kipigo kutoka kwa Wolves ni kipigo cha tatu mfululizo kwa Liverpool.Walitoka kupigwa na Swansea,wakapigwa EFL na Southampton hatimaye Wolves nao wamekuja kuwafunhasha virago katika michuano hii ya FA.Na Klopp amesema “wakulaumiwa ni mimi.”
Wakiwa wametoka kupigwa mechi hizo tatu,inaonesha mechi zinazofuata za Liverpool ni ngumu zaidi kuliko zilizopita.Mechi zinazokuja za Liverpool zitakuwa dhidi ya timu tatu za juu kwenye ligi ambazo ni Chelsea,Arsenal na Tottenham.
Wengi walitarajia kurudi kwa Coutinho itakuwa suluhisho kwa Liverpool.Lakini hali inaendelea kuwa mbaya.Tayari wachambuzi wa mambo ya soka wameanza kumnyooshea mkono Klopp kwa madai kwamba anawafanya wachezaji wa Liverpool kuchoka.Liverpool ndio timu inayoonekana kupress zaidi,toka mwanzo wa ligi wanaonekana kushambulia kwa kukimboa sana na hii inaonesha sasa wamechoka.Liverpool ndio timu inayoongoza kwa kukimbia zaidi Uingereza.
Msimu huu Liverpool wamekimbia 2579 kilomita na hii inaifanya iwe timu iliyokimbia kilomita nyingi zaidi.Man City nao wanawafuatia Liverpool 2517 kilomita huku West Brom nao wakiwa nafasi ya tatu wakikimbia kilomita 2508.
Kukosekana kwa mshambuliaji wao Sadio Mane huenda pia inawafanya kukosa mtu muhimu wa kukimbia na mipira mbele.Lakini sasa Mane nae anaonekana yuko njiani kurudi Uingereza baada ya timu yao ya Senegal kutolewa katika mashindano ya AFCON.