Kufuatia kukamilika kwa kazi ya kutandika reli mpya katika eneo Korofi kati ya stesheni na Ilala block post na karakata Uongozi wa Kampuni ya reli Tanzania unawajulisha wasafiri wa treni ya mjini commuter train iendayo Pugu kuwa safari ya tatu itaanza tena January 25 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es salaam mkuu wa usafirishaji TRL Rashidi Ng’wani amesema treni itaanza safari zake kuanzia kituo kikuu cha Dar es salaam saa 2:15 usiku na kuwasili Pugu 3:10 usiku.
Hata hivyo ameeleza kuwa kwa awamu ya safari za asubuhi safari zitaendelea kuwa mbili ili kupisha kazi ya ukarabati wa njia ya reli ambapo kazi hiyo huanza saa 3:15 asubuhi hadi saa 8:15 mchana kila siku za kazi na inatarajiwa kukamilika baada ya wiki kumi.
Aidha Ng’wani amesema ukarabati huo umelenga kubadilisha reli ndogo za ratili 60 na kuweka reli kubwa za ratili 80 ambazo ni imara na kuwezesha kutembea kwa usalama zaidi pia kuondoa kero kwa abiria ikiwemo vumbi kwenye mabehewa ambapo njia itawekwa kokoto za kutosha ambazo hazina vumbi.