Nay wa Mitego na lulu Diva
Muuza sura kwenye video za Kibongo na msanii mpya wa bongo Fleva, Lulu Abbas maarufu 'Lulu Diva' amefunguka na kuweka wazi kuwa aliamua kumuacha rapa Nay wa Mitego kutokana na tabia zake za hapa na pale.
"Niliamua kumwaga Nay wa Mitego kwa kuwa hajatulia, akiona kila mwanamke macho yanamtoka na kumuwaka, ila naweza kumzungumzia kuwa Nay wa Mitego ni mtu poa sana ukimuona kwenye TV na maisha anayoishi yuko tofauti sana, msafi sana, anajali ni mshikaji poa na ni mtu muelewa sana ila tu ni mtata sana na hizo tabia zingine za kibinadamu ambazo mimi zilinishinda na kuamua kumuacha" alisema Lulu Diva
