Mahakama Kisutu yafuta kesi ya umeya Kinondoni

Benjamini Sitta 

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi  ya matokeo ya umeya wa Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Mahakama imefuta kesi hiyo leo  baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowekwa na meya wa manispaa hiyo, Benjamini Sitta kupitia kwa wakili wake, Baraka Nyambita.

Kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2016 ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea umeya katika manispaa hiyo kupitia Chadema, Mustafa Muro na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya  unaibu meya kupitia chama hucho, Jumanne Mbunju.
Mpya zaidi Nzee zaidi