Mkenya ajiunga na klabu ya China kwa ksh. 467m

Mshambuliaji wa Kenya Michael Olunga
Mshambuliaji wa Kenya Michael Olunga

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na klabu iliopandishwa daraja katika ligi ya China Guizhou HengFeng Zhicheng kwa kitita cha fedha kisichojulikana kutoka kwa klabu ya Djurgadens IF ya Sweden.

Olunga mwenye umri wa miaka 22 aliachiliwa na Djurgadens IF baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana.

Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, Olunga alikuwa amesalia na miaka mitatu katika kandarasi yake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Gor Mahia na Tusker pia amekuwa akisakwa na klabu ya Urusi ya CSKA Moscow.

Guizhou Zhicheng Hengfeng ilikuwa imemuulizia mshambuliaji huyo na iliripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha shilingi milioni 467 zilizodaiwa na Djugardens.

Olunga pia alikuwa amevutia klabu ya Uturuki ya Galatasaray.

Mchezaji huyo aliifungia Gor Mahia mabao 19 katika msimu wa 2015, na kuwasaidia kushinda taji la 15 la KPL pamoja na taji la Top 8 kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Sweden.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia