Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda amezindua jengo jipya la kisasa la huduma ya mama wajawazito na watoto kitengo cha Dharura katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala, ambalo litasaidia utoaji huduma za Upasuaji kwa akina mama wajawazito na kupunguza Msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.
Akizungumza kabla ya kuzindua jengo hilo lillojengwa kwa udhamini wa Gsm Foundation ya jijini dsm amesema kukamilika kwa jengo hilo kutaokoa maisha ya kina mama na watoto hasa wale wanaopata dharura ya kufanyiwa Upasuaji ambapo kwa wakati mmoja linaweza kutoa huduma kwa akina mama 10 hadi kumi na watano.
Amesema GSM foundation imeonyesha uzalendo wa kweli kwa kusaidia jamii hususan huduma za Afya ya mama na mtoto kwa kujenga jengo hilo ambalo limegharimu kiasi cha shilingi million 420.
Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Nkungu Daniel amesema Hospitali hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa akina mama wajawazito kati ya 100 hadi 120 kwa siku hali inayosababisha kuwapeleka muhimbili kutokana na msongamano.