Mourinho asema Martial anakipaji kikubwa sana

Ajenti wa mchezaji huyo raia wa Ufaransa ameripotiwa akisema kuwa anaangalia chaguo la mteja wake kwenda kuchezea Sevilla.

Martial ambaye ana umri wa miaka 21, msimu uliopita alikuwa mchezaji mwenye mabao mengi katika klabu ya United msimu alikuwa na mabao 17 ,lakini bao lake la kusawazisha siku ya Jumamosi lililosaidia United kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Middlesborough ni la tano msimu huu.

”Ni mchezaji ambaye anaweza kuwa maarufu sana” ,alisema Mourinho.

”Martial alicheza ,alisaidia na kufunga.Alipigania mipira,alikuwa na lengo na najua anakipaji kikubwa”.

Martial ambaye alijiunga na United akitokea Monaco kwa pauni milioni 36 mwaka 2015 alikuwa kiungo muhimu baada ya timu yake kutoka nyuma na kuilaza Middlesborough.

Alifunga goli kunako dakika ya 85 kabla ya Paul Pogba kufunga bao la ushindi kwa kichwa dakika moja baadaye.
Mpya zaidi Nzee zaidi