Msafara wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani ulizuiliwa na wakazi wa Kijiji cha Singisi huku wakiwa na mabango wakilalamikia uharibifu unaofanywa na tembo.

Makani aliyekuwa akitoka kwenye shamba la mwanakijiji lililoharibiwa na tembo, ilimlazimu kuzungumza na wakazi hao.
Mwakilishi wa wakazi hao, Mang’asa Mkira ameiomba Serikali kuchukua hatua kwa kuwa mazao yao huharibiwa na tembo na hawalipwi fidia.
Mkazi wa Kijiji cha Makundusi, Mrimi Nyamhanga amesema amelazimika kuhamisha familia yake baada ya tembo kuvamia nyumba yake, kuezua paa na kubomoa kuta wakiwa wamelala.