Msemaji wa rais mteule Gambia amesema kwamba shughuli ya kumuapisha rais zitaendelea kama kawaida huku Jammeh akisema hang’oki madarakani

Msemaji wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow,amesema kwamba shughuli ya kumuapisha rais huyo itaendelea kama ilivyopangwa mnamo Januari 19.

Tangazo hilo limetolewa wakati rais Yahya Jammeh akisisitiza kwa mara nyingine kwamba hatoondoka madarakani.

Msemaji wa Adama Barrow Mai Fatty ameliambia shirika la habari la AFP mjini Dakar Senegal kwamba Muhula wa rais Jammeh utamalizika Januari 19 na siku hiyo hiyo ataapishwa rais mteule Adama Barrow kuanza hatamu ya uongozi wake na hakuna kitakachobadilisha mpangilio huo.

Imethibitishwa pia hapo jana na rais wa Senegal Macky Sall kwamba ameridhia ombi la rais wa Liberia Ellen Johnson Sirlif la kumkaribisha nchini Senegal Bw. Barrow hadi itakapofika siku ya kuapishwa kwake.

Hata hivyo msemaji wa Barrow hakutowa maelezo kuhusu wapi ataapishwa rais mteule na chini ya mazingira gani hasa kutokana na kutarajiwa kukabiliwa na hali ngumu katika kurudi kwake nchini Gambia.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia